Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tahadhari ya Mlipuko wa Ugonjwa wa Surua Dodoma

Surua Tahadhari ya Mlipuko wa Ugonjwa wa Surua Dodoma

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ametoa tahadhari kwa Wakazi kuhusu Mlipuko wa Ugonjwa wa Surua na kuwataka Watoto wenye Umri chini ya Miaka 5 kupelekwa kwenye Zahanati au Vituo vya Afya ili kupatiwa Chanjo ya Ugonjwa huo

Surua (Measles) ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vinavyosambazwa baada ya Mtu mwenye Ugonjwa kukohoa au kupiga chafya. Watu ambao hawajapata Chanjo wapo katika hatari kubwa ya kuambukizwa.

YAH: TAARIFA YA MLIPUKO WA UGONJWA WA SURUA KATIKA JIJI LA DODOMA​

Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.

Mnajulishwa kuwapo na mlipuko wa Ugonjwa wa Surua katika Jiji la Dodoma. Na hili linatokana na sampuli zilizochukuliwa kuthibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Suru ana hivyo kufanya Wilaya yetu kuwa na mlipuko wa Ugonjwa wa Surua.

Kwa barua hii mnaelekezwa kuwajulisha wananchi kuchukua tahadhari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa surau na pia kuwapeleka Watoto wenye umri chini ya miaka 05 katika Zahanati vituo vya Afya kupatiwa chanjo ya ugonjwa huo.

Nawatakia utekelezaji mwema.

Patrick Bashemara Kny; MKURUGENZI WA JIJI DODOMA​

Chanzo: www.tanzaniaweb.live