Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tafiti: Unatakiwa kula 'dinner' saa 4 kabla ya kulala

Eat Dinner Kula 'dinner' saa 4 kabla ya kulala

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu wa masuala ya afya nchini Marekani wamesema muda mzuri wa kula chakula cha jioni kwa mtu yeyote unatakiwa kuwa kati ya dakika 180 (saa tatu) au dakika 240 (saa nne) kabla ya kupanda kitandani kulala ili kuupa mwili nafasi ya kufanyia kazi chakula hicho kama inavyotakiwa.

Wataalamu hao wamesema saa tatu au saa nne kabla ya Mtu kulala ndio muda sahihi zaidi kwakuwa mwili unaweza kukifanyia kazi kama inavyotakiwa ikiwemo mmeng’enyo lakini pia kunamuepusha Mtu kukumbana na magonjwa mbalimbali.

Utafiti huu unakazia ripoti ya Julai mwaka 2018 ambayo ilisema Watu wanaokula chakula cha jioni kabla ya saa tatu usiku au angalau saa mbili kabla ya kulala wana hatari ya chini ya 20% kupata saratani (cancer) ya matiti na kibofu kuliko wale wanaokula chakula mida ya saa nne usiku au wale wanaokwenda kulala muda mfupi baada ya kula.

Ushauri mwingine wa Wataalamu umesema kunywa maji baada ya chakula ni muhimu kwa kila Mtu lakini kila mmoja anapaswa kuzingatia kuwa anashauriwa kufanya hivyo angalau dakika 30 baada ya kumaliza kula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live