Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tafiti: Uingereza Kuna uhaba mkubwa wa mbegu za kiume

Erectile Dysfunction Treatments Which Is Righ L Wc9zsq.jpeg Kuna uhaba mkubwa wa mbegu za kiume

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Mtandao wa raconteur.net, kuna uhaba mkubwa wa mbegu za kiume barani Ulaya; hasa nchini Uingereza.

Inaelezwa kuwa, maelfu ya sampo za mbegu za kiume zimekuwa zikiingizwa barani humo kutokea mabara mengine hasa Afrika kila mwaka kutokana na uhitaji mkubwa wa wanawake wanaohitaji kupandikiza mimba.

Kwa mujibu wa Dokta Chale; daktari maarufu wa mambo ya uzazi jijini Dar anayeandikia Gazeti la IJUMAA anasema; “Katika hali ya kawaida, mimba hutunga kupitia tendo la ndoa pale mbegu za kiume au manii zinapoungana na yai la mwanamke.

“Kupandikiza mimba au kwa kimombo ni In Vitro Fertilization (IVF); ni mchakato wa kuunganisha yai la mwanamke na mbegu za mwanaume nje ya mwili wa binadamu katika maabara kisha kurudishwa kwenye mwili wa mwanamke ili mimba ikue.”

Mwaka jana, Wizara ya Afya nchini Tanzania ilitangaza kuwa hospitali kuu ya rufaa ya Muhimbili imeanza kutoa huduma za upandikizaji mimba kwa wanawake.

Uhaba huo unakuja kufuatia wanaume wa Kingereza kugoma kuchangia mbegu ili kuwekwa kwenye benki ya mbegu za kiume ya nchi hiyo.

Profesa Allan Pacey wa Chuo Kikuu cha Sheffield cha Uingereza anasema; “Ndiyo kuna uhaba, lakini uhaba huu siyo kama tuliokuwa nao miaka 10 au 20 iliyopita.”

Inaelezwa kwamba kuna ongezeko kubwa la wanawake wanaotaka kupata watoto bila kujamiiana na hata hapa Tanzania, msanii Malkia Karen amekiri kufanya hivyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Mtanzania aliyeko nchini Uingereza, tatizo hilo siyo la Uingereza pekee, bali ni kwa nchi nyingi barani Ulaya na duniani hasa kwa nchi zilizoendelea kisayansi na vijana mashababi wa Kiafrika wanakimbilia humo kwa ajili ya kuchangia mbegu za kiume na kupata mamilioni ya pesa.

“Hata hivyo, hivi sasa kuna kampeni za chinichini kwamba, wasichukue mbegu hizo kwa wanaume wa Kiafrika ambazo zinapatikana kwa wingi kutokana na uzalishaji wa miili yao kwani kuna kila dalili baada ya miaka 100 mbegu ya Kiafrika ikawa imeongezeka mno na kupoteza kizazi cha wazungu,” anasema na kuongeza;

“Huu ni mjadala mzito mno hasa kwa tasnia ya sayansi na baiolojia kwa sababu tatizo limekuwa kubwa, benki za mbegu za kiume zina uhaba mkubwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live