Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora yapewa barakoa za mil. 20/-

Tabora.webp Tabora yapewa barakoa za mil. 20/-

Mon, 4 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMPUNI ya Usafirishaji ya Athwal (ATT) ya mjini Tabora, imetoa msaada wa barakoa zenye thamani ya Sh. milioni 20 kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora.

Msaada huo ulikabidhiwa jana na Ofisa Usafirishaji wa ATT, Godfrey Tarimo, kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ili kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

Alisema kampuni hiyo ambayo inatoa huduma za usafirishaji ndani na nje ya Tabora, imeamua kutoa msaada huo ili kusaidia katika mapambano dhidi ya virusi vya corona mkoani Tabora.

Akipokea msaada huo, Mwanri, alisema umekuja wakati muhimu ambapo Taifa liko katika vita ya kudhibiti ugonjwa wa Covid- 19 usiendelee kusambaa.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema wadau wote mkoani humo wanapaswa kuungana katika vita ili hatimaye waweze kuushinda ugonjwa wa Covid-19.

Alisema msaada huo walioupokea baada ya kuthibitishwa na wataalamu wa sekta ya afya kuwa ni za viwango, na kwamba zitagawanywa katika wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kuwasaidia watoa huduma za afya, ambao wanasaidia kukabiliana na virusi hivyo pamoja watu wengine ambao hawana uwezo wa kuzinunua.

Mwanri alitoa wito kwa wadau wengine wanaoendesha shughuli zao, zikiwamo za biashara kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya corona.

Katika hatua nyingine, Mwanri ameagiza maeneo yote yanayotoa huduma kama sokoni na stendi kufungwa vipasa sauti ili watu wanaofanyia kazi maeneo hayo waendelea kupata elimu ya kujikinga na Covid -19.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wasafiri na wafanyabiashara wanaokuwapo katika maeneo hayo wanapata elimu sahihi ya kukabiliana na kujikinga virusi vya corona.

Mwanri alitoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa masoko, stendi na wajane wakati akiongoza timu ya wataalamu wa afya kutoa elimu ya kujikinga na Covid -19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live