Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi ya Utalii ya chemchem yatoa baiskeli za milioni 21 kwa walemavu Babati

40a18d97aeed4fa1cd03d0163f23fd0a Taasisi ya Utalii ya chemchem yatoa baiskeli za milioni 21 kwa walemavu Babati

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amekabidhi baiskeli 31 kwa walemavu zenye thamani ya sh 21 milioni.

Baiskeli hizo zimetolewa na Taasisi ya Uhifadhi ya Chemchem ambayo imewekeza Utalii wa picha na hoteli Wilayani Babati.

Akizungumza leo wakati akikabidhi Baiskeli hizo, Mkirikiti alishukuru taasisi ya Chemchem kutoa Msaada huo na kutaka iendelee kusaidia jamii mkoa wa Manyara.

"Tunashukuru kwa Msaada huu lakini isiwe mwisho endeleeni kutoa kama mchango wenu kwa jamii na mimi leo ntatoa mchele kwaajili wa sikukuu kwa walemavu hawa pia fedha kidogo za kuwasaidia," amesema.

Mkurugenzi wa chemchem Nicolas Negri amesema Msaada huo ni sehemu ya baiskeli 242 ambazo wanakusudia kutoa kwa walemavu.

"Biashara yetu kubwa sisi ni Utalii hivyo kama tukiendekea kuhifadhi mazingira na kutunza wanyama tutaendelea kupata Watalii na kunufaika wote," amesema.

Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara ina jumla ya walemavu 1811 wa aina mbalimbali ikiwepo walemavu wa viungo 249.

Chanzo: habarileo.co.tz