Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMDA yawafunda wakuguzi wa dawa na vifaa tiba Shinyanga

Td TMDA yawafunda wakuguzi wa dawa na vifaa tiba Shinyanga

Wed, 12 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wakaguzi hao dawa na vifaa tiba, kutoka Halmashauri zote za mkoa huo wakiwamo wa famansia, waratibu wa huduma za maabara, na wataalamu wa mifugo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi, Dk. Edga Mahundi, amewataka wakaguzi hao kuzingatia maadili wakati wa ukaguzi, kufuata sheria, kuacha jeuri, matusi, kejeli, pamoja na kutopokea Rushwa kwa watuhumiwa.

Amesema wakaguzi hao wakifanya kazi yao vizuri, hakutakuwa na uuzwaji wa madawa holela wala uingizwaji, yakiwamo maduka bubu na maabara, hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa nchi kuwa salama, pamoja na kulinda afya za wananchi sababu ya kutotumia madawa yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu.

“Naombeni sana wakaguzi wa dawa na vifaa tiba mkoani Shinyanga, fanyeni kazi yenu kwa weledi ili kudibiti matumizi na uingizwaji wa dawa holela na vifaa tiba, sababu Mkoa huu unapakana na nchi jirani kwa upande wa Kahama, hivyo kuna hatari kubwa ya matumizi ya dawa zisizo sajiliwa, duni, bandia, pamoja na zilizomaliza muda wake,”amesema Mahundi.

“Dawa na vifaa tiba visivyo faa zikiingia hapa nchini, ni hasara kubwa kwa Serikali na kuathiri shughuli za uchumi sababu ya wananchi kuwa na afya duni, hivyo wakaguzi msiwe na mdhaha kwenye zoezi la ukaguzi,”ameongeza.



Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yudas Ndugile, amewataka wakaguzi hao kudhibiti pia uibwaji wa madawa ya Serikali na kuuzwa kwenye maduka binafsi, huku zingine zikisafirishwa nchini Uganda, au dawa za Uganda kuingia hapa nchini ambazo hazina usajili.

Pia ametoa mbinu kwa wakaguzi hao. ili wapate kufanikiwa kudhibiti matumizi ya madawa holela na uingizwaji vikiwamo vifaa tiba, ni vyema wakafanya kazi karibu na viongozi wa Serikali za Mitaa, ili kuwapatia taarifa mbalimbali za watu ambao wanaihujumu Serikali yakiwamo na maduka bubu ya dawa na maabara.

 
Chanzo: ippmedia.com