Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMDA yateketeza dawa za Sh180 milioni

Fake Drugs Burnt TMDA yateketeza dawa za Sh180 milioni

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imeteketeza shehena ya dawa za aina mbalimbali ziliyokwisha muda wa matumizi kwa binadamu tani 10 zenye thamani ya Sh180 milioni.

Meneja wa TMDA Kanda, Anitha Mshighati amesema leo Jumatatu Julai 6, 2022 wakati wa zoezi la uteketezaji lililofanyika katika Hosptali ya Mission ya Igongwe Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Amesema kuwa shehena hizo zilipatikana kwa mkazi wa Uyole jijini Mbeya (jina limehifadhiwa) huku akiweka bayana kukamatwa kwake kulitokana na taarifa kutoka kwa wananchi baada ya kuona uingizwaji wa shehena za madawa katika eneo lisilo rasmi.

''Madawa yaliyoteketezwa ni pamoja dawa za sindano aina tofauti ambazo zilikuwa ni hatarishi kwa matumizi ya binadamu ambapo watu wangepatiwa matibabu yangepelekea kupata madhara na hata kupoteza maisha ''amesema.

Ofisa wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Hans Cheyo amesema kuwa wamekuwa wakizingatia vigezo vya matanuru yanayo teketezewa taka hatarishi hususani dawa ziliyokwisha muda pasipo kuleta madhara kwa wananchi.

''Kwa leo tumekuja kutekeleza katika Hosptali ya Mission ya Igongwe tumeona vigezo na kutokuwepo kwa athari kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kununua madawa kwenye maduka au kupata ushauri kwa wataalam ili kuepuka na na matumizi ya dawa zilizokwisha muda na kuleta madhara kiafya.

Mkazi wa Kiwira Ally Mwakisile amesema kuwa kuna kila sababu kwa TMDA kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa maduka ya dawa muhimu ili kuwasaidia wananchi kununua dawa feki au zilizokwisha  muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live