Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMDA yateketeza dawa na vifaa tiba vya zaidi ya Milioni 200

Tm.jpeg Baadhi ya bidhaa zilizo teketezwa

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kusini kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imeteketeza dawa na vifaa tiba ambazo zimekwisha muda wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni 205/= [mia mbili na tano]

Kazi hiyo imefanyika katika hospitali ya Wilaya ya Liwale chini ya usimamizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri kupitia idara ya Afya baada ya kupata kibali kutoka kwa mhakiki mali wa Serikali.

Uteketezaji wa dawa na vifaa tiba hufanyika kwa kufuata taratiba za Serikali na utunzaji wa mazingira,aidha wakati wa kufanya uteketezaji huo kuna kuwepo na ushirikishwaji wa idara ya mazingira, polisi na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live