Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMDA yaonya matumizi ya Viagra, dawa za kutoa mimba

DSC 1120 TMDA yaonya matumizi ya Viagra, dawa za kutoa mimba

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlama ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) imesema bidhaa ya dawa ni hatari hivyo ni muhimu kabla hujatumia kwanza kupima,kupata ushauri wa daktari ili uambiwe kama unatakiwa kutumia dawa.

Mwito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa TMDA Adam Fimbo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Amesema utumiaji wa dawa holela kwa mfano dawa kutoa mimba umekuwa mkubwa na wanaotumia zaidi dawa hizo ni wanafunzi na wanawake wenye umri mdogo lakini madhara yake katika jamii ni makubwa.

Pia kumekuwa na matumizi makubwa ya dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu kwa jina la Viagra ambapo dawa hizo zimekuwa zikitumika ndivyo sivyo.

“Kuna watu wengi wamekuwa wakizitumia , tumepata ripoti mbalimbali kuna ambao wanapoteza maisha , mwito wangu mkubwa usitumie dawa hizo bila kupata ushauri wa watalaamu , lazima upate ushauri wa watalaamu ili wakushauri namna bora ya kutumia dawa.

“Matumizi ya dawa hizi jamii ya Viagra yamekuwa makubwa sana nchini Tanzania , tunafanya tafiti kuangalia matumizi yake yapo kwa ukubwa na kwa kiwango gani,”amesema Fimbo.

Amefafanua baada ya kufanya utafiti huo lengo lao litakuwa ni kutoa elimu zaidi kwani wanazitumia isivyotakiwa.

“Kwasaabu matukio mengi ya watu kupoteza maisha na kupata mashinikizo ya damu yameongezeka.

“Hivyo tutaendelea kuelimisha umma dawa hizi hazipaswi kutumiwa kiholela hasa kutokana na madhara yake kwa mwili wa binadamu.Kuhusu dawa za kutoa mimba maarufu P2 nazo zimekuwa zikitumiwa sana hasa na watoto wa shule kutoa mimba.

“Hivyo tumeziwekea mkakati wa kudhidhiti, tunatoa elimu kwa watoto wetu na wanawake wengine wa marika madogo waache kuzitumia kiholela kwasababu zimekuwa zikisababisha vifo ambavyo havijatarajiwa,”amesema.

Akizungumzia maonesho hayo ,Fimbo amesema wanatumia kuwaleza wananchi yale ambayo yanafanywa na TMDA hasa katika kuhakikisha wanakuwa salama.

“Kupitia maonesho haya tunawaambia yale ambayo TMDA tunayafanya hasa katika kulinda afya ya jamii yetu, ulindaji wa afya ya jamii unahusisha usajili bidhaa tangu zinapoingia kwenye soko la Tanzania.

“Ili mtu anapotumia bidhaa ziwe ni zile ambazo zimethibitishwa na TMDA na zina ubora , ufanisi na usalama unaotakiwa kwasababu dawa ni bidhaa za sumu ambazo zinaweza kumdhulu mtu na hivyo zinahitaji kutumika vizuri kwa kufuata masharti ya daktari na watalaam wengine wa afya.

Amefafanua kupitia mifumo waliyoiweka wanazo ofisi za kanda ambazo zinafanya ukaguzi na dawa yoyote ambayo inaingia Tanzania kwa kuhakikisha inakaguliwa.

“Kwa mfano juzi tu tumefanya operesheni na tumekamata mzigo mkubwa wa dawa ambazo zilikutwa kwenye duka ambalo halijasaliwa na TMDA, kwa hiyo hayo ni sehemu ya majukumu yetu makubwa.

“Tumekuwa tukiyafanya kila siku na lengo kubwa ni kulinda afya za watanzania kwa hiyo tuko hapa Sabasaba kwa ajili ya kueleza hayo wananchi wanaofika hapa wafahamu na kujilinda wao wenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live