Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMDA kuchunguza aliyechomwa sindano Arusha

Sindano Vifoooo TMDA kuchunguza aliyechomwa sindano Arusha

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imesema, inafanya uchunguzi wa tukio la mwananchi aliyedai kuchomwa sindano katika duka la dawa muhimu na kuungua vidole vya mkono wa kushoto.

Tukio hilo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Mei 8, 2023 ambapo Ester Mkombozi alionekana kwenye picha mjongeo akidai vidole vyake vya mkono wa kushoto vimeungua baada ya kuchomwa sindano katika duka la dawa alilolitaja kwa jina la El-shadai Medics lililopo Kata ya Ngulelo jijini Arusha.

Kupitia video hiyo, jana Mei 11,2023 TMDA kwenye taarifa iliyotolewa kwa umma ilieleza kwamba, baada ya kuiona video hiyo ilifuatilia na kumpata Easter na tayari wameanza kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo na itatoa taarifa kamili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live