Maambukizi ya tezi dume yameongezeka miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani ilipokuwa nadra kusikia mtu amepata tatizo hili.
Wachache walio-kuwapo ni watu wazima. Wakati hamasa ya kupima ikiongezeka, changamoto mpya nazo zinaibuka. Iliyopo sasa ni gharama kubwa za matibabu yake.Matibabu ni ghali na mara nyingi wagonjwa hushauriwa kufanyiwa upasuaji ambao gharama zake hazishikiki pia hasa kwa wenye kipato cha chini.
Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa tezi dume, wata-alamu wanasema huhitajika kurudia tena baada ya miaka mitano hivi. Lakini, ipo njia nyingine ya kukabiliana na maradhi haya nayo ni tiba mbadala. Kwa kutumia dawa za asili, tatizo hili linaweza kwisha endapo mgonjwa atafuata masharti bila kufanyiwa upasuaji, tena kwa gharama nafuu. Wataalamu wa afya ya figo na kibofu cha mkojo wanasema uvimbe usio wa saratani ambao husababisha tezi dume kupanuka ndio unaosababisha ugonjwa huu ambao huwapata wanaume tu.
Uvimbe huu ukiongeze-ka au kutanuka hasa kwa wanaume wenye zaidi ya miaka 60, hutatiza kukojoa hivyo dalili za ugonjwa huu unazidi kuongezeka duniani kuwa dhahiri.Tezi dume ni kiungo kido-go na sehemu ya uzazi wa wanaume inayopatikana chi-ni ya kibofu, mbele ya njia ya mkojo. Tezi dume ndiyo hutoa maji yabebayo mbegu (manii) za kiume.
Pia Soma
- Jifunze kuwa mkweli kwa daktari wako
- PIRAMIDI YA AFYA: Ugonjwa wa baridi yabisi na karaha kwa wazee
- Mila zinavyochochea utoaji mimba Magu
- Maajabu ya ndimu, limau katika kuongeza damu mwilini
Tiba hii hupatikana kwa kuchangan-ya tangawizi ya unga, kamun aswadi, khurinjani, albatisoda, hulba na sufa. Vyote viwe vya unga. Ukishavichanganya, unapaswa kutu-mia kijiko kimoja kwenye uji au chai kutwa mara tatu kwa mwezi mzima.