Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFDA: Panadol ni salama kwa matumizi

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Teaser title: TFDA: Panadol ni salama kwa matumizi

Summary: Imetoa ufafanuzi huo baada ya kusambaa kwa video ikieleza dawa hiyo ni feki

 

Bakari Kiango, Mwananchi

[email protected]

Dar es Salaam. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema dawa aina ya Panadol ni sahihi kwa matumizi kama zilivyo dawa nyingine.

Kauli hiyo ya TFDA imetolewa leo Juni 29, 2018 baada ya hivi karibuni kusambaa video katika mitandao ya kijamii zikionyesha mashaka kuhusu usalama wa dawa aina ya Paracetamol yenye jina la kibiashara la Panadol.

Video hiyo ilionyesha kuwa dawa hiyo yenye muundo wa vidonge,  ikimwagiwa maji inageuka kuwa kitambaa.

Lakini leo Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Agness Kijo amewaeleza waandishi wa habari kuwa taarifa hiyo si sahihi na panadol ni salama kwa matumizi.

“Bidhaa inayohusishwa na dawa tajwa ni kitambaa ambacho kimetengenezwa kwa muundo wa vidonge na juu hakuna lebo ya panadol wala paracetamol kama inavyoelezwa kwenye video inayosambaa,” amesema Kijo.

“Bidhaa hii hutumika zaidi katika mahoteli au maeneo mengine. Kufuatia uvumi huu mamlaka imefanikiwa kumpata mtu  anayedaiwa kusambaza video hiyo na anaendelea kuhojiwa kuhusu upotoshaji  wa wazi kuhusu dawa hii,”amesema.

Kijo amewahakikishia wananchi kuwa TFDA itaendelea kufuatilia usalama wa dawa kwenye soko ili kuhakikisha inaendelea kuwa salama kwa watumiaji.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz