Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS: Ni hatari kutumia dawa, pombe kulainisha nyama

Nyama Marination Nyamaaa TBS: Ni hatari kutumia dawa, pombe kulainisha nyama

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

hirika la Viwango Tanzania (TBS), limeionya jamii kuacha kutumia dawa na pombe kali kulainisha vyakula, hususani nyama kwani ni hatari kwa afya ya mlaji.

Hayo yamesemwa leo Februari 13, 2024 na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Kufanya tathmini vihatarishi vya chakula kutoka TBS, Ashura Katunzi akizungumzia usalama wa chakula.

Amesema, jamii ya Watanzania wanapaswa kutumia malighafi zilizo sahihi katika kulainisha vyakula na sio kutumia dawa, vinywaji vikali, ili kulainishia akitolea mfano nyama ya utumbo.

“Baadhi ya watu wanaweka dawa za hospitali kwenye utumbo wakati wa kuchemsha, ili uive haraka, hii si salama kiafya, au wengine wanatumia vinywaji vikali kulainisha nyama ya kuchoma,” amesema.

Amesema njia hiyo isiyo halali huashiria sumu na kusababisha hatari kubwa kwa afya ya walaji, huku madhara yake yakitajwa kuwa ni athari kwenye ubongo, ini na figo na hivyo kusababisha ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa upande wa Kaimu Meneja wa Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria kutoka TBS, Moses Mbambe amesema katika kudhibiti ubora wa chakula wanazingatia mambo matatu, uhamasishaji wa uzingatiaji wa viwango katika usindikaji, utayarishaji na uuzaji wa bidhaa za chakula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live