Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TB bado tishio nchini

E068cea7cc74a3100e7eac294bec5a87 TB bado tishio nchini

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UGONJWA wa Kifua Kikuu bado umeelezwa kuwa tishio nchini huku Tanzania ikitajwa kuwa miongoni mwa nchi 30 duniani zenye maambukizi ya juu ya ugonjwa huo sawa na asilimia 87.

Hayo yameelezwa na Dokta Zuwena Kondo, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP).

Alisema kwa sasa mlipuko wa janga la Corona limefunika ugonjwa wa TB lakini bado ugonjwa huo upo juu na takwimu za mwaka 2018 watu 142,000 waliugua ugonjwa wa kifua kikuu nchini kati yao wanaume 79,500 na wanawake 39,800 huku watoto ni 22,700.

Dokta Zuwena alisema katika mwaka huo wa 2018 waliopoteza maisha ni watu 22,000 kati yao watu 16,000 waliokuwa na VVU walikufa kutokana na TB.

“Kati ya wagonjwa wapya 142 waliokadiriwa kuugua TB nchini mwaka 2018, ni 75,00 sawa na asilimia 53 ndio waligunduliwa na kuwekwa kwenye matibabu. Hii inamaanisha kwamba kuna wagonjwa 67,000 hawakuweza kugunduliwa, hii ni hatari kusambaza zaidi maambukizi.” alisema

Aidha alisema kifua kikuu kwa watoto pia ni changamoto kwani mwaka 2018, Watoto 22,700 waliumwa TB nchini na kwamba watoto mara nyingi huwa wanasahaulika na watoa huduma za afya kwa sababu ugunduzi wa TB kwa watoto huwa na changamoto.

Hata hivyo Dokta Zuwena alisema mkakati wa serikali ambao unakwenda na malengo ya milenia ni kupunguza janga la Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2035.

Alisema kwa sasa serikali imeweka mkakati wa kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuwaelimisha kuwa ugonjwa wa TB unapona, na pia sio kila anayeugua TB ana anaishi na VVU na si kila mwenye VV anaugua TB ili kupunguza unyanyapaa ambao unawafanya wagonjwa wasijitokeze kwa wingi kwa kuhofia jamii itawatenga.

Aidha alisema watu wengi pia hawana uelewa mkubwa wa dalili za TB ambapo alisema baadhi ya dalili hizo ni kukohoa kwa wiki mbili au zaidi na kutoa makohozi yenye mchanganyiko wa damu, kutoaka jasho kwa wingi hasa wakati wa usiku hata maeneo ya baridi, kupata homa za mara kwa mara wakati wa jioni kwa wiki mbili au zaidi na kupungua uzito.

“Watu bado hawana uwelewa mkubwa wa dalili za kifua kikuu, bado tunaendelea kutoa elimu ili mtu akiona dalili hizo basi awahi hospitali, matibabu ni bure, kwani kugundua ugonjwa mapema, unapata matibabu sahihi kwa miezi sita ukifuata masharti unapona kabisa,” alisema

Hata hivyo alisema changamoto kubwa kwa sasa iliyopo ni uwezo wa ugunduzi kutokana na jiografia ya nchi, kuna maeneo mengi bado hayajafikiwa.

“Nchi yetu ni kubwa, vigunduzi vipo hospitali za wilaya, lakini kuna asilimia kubwa maeneo mengine hawajapata vifaa, mgonjwa akiambiwa sampuli zimesafirishwa anakata tamaa na kukimbilia kwa waganga.

Chanzo: www.habarileo.co.tz