Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKWIMU: Kila baada ya dakika 1 mtu mmoja hufariki kwa UKIMWI

HIV TEST.jpeg Kila baada ya dakika 1 mtu mmoja hufariki kwa UKIMWI

Thu, 28 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takwimu mpya za UNAids zinaonesha kuwa kila dakika alikufa mtu mmoja kutokana na ugonjwa unaohusiana na Ukimwi mnamo 2021.

Pia inakadiria kuwa "kila dakika mbili mwaka wa 2021, msichana au mwanamke kijana alikuwa ameambukizwa HIV".

Ripoti hiyo - iliyopewa jina la In Danger - ilitolewa katika mkutano wa mwaka huu wa Global UNAids huko Montreal, Canada.

Ulimwenguni, wanawake na wasichana walichangia asilimia 49 ya maambukizi mapya mwaka 2021.

Hata hivyo, Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, walichangia asilimia 63 ya maambukizi mapya katika mwaka huo huo.

Takribani watu milioni 1.5 waliambukizwa HIV mwaka jana kulingana na data.

Ripoti hiyo inaonesha zaidi kwamba maambukizi mapya yanaongezeka ambapo hapo awali yamekuwa yakipungua.

"Takwimu zilizofichuliwa katika ripoti hii zitasumbua na kushtua - lakini ripoti hiyo sio sababu ya kukata tamaa. Ni wito wa kuchukua hatua.

Kushindwa kunaweza kuwa kubaya, lakini sio kuepukika. Tunaweza kukomesha Ukimwi ifikapo 2030.

Lakini 'curve' haitajipinda yenyewe. Tunapaswa kuishusha,” alisema Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAids.

Ulimwenguni kuna watu milioni 38.4 wanaoishi na HIV. Mashariki na kusini mwa Afrika inabeba mzigo mkubwa zaidi duniani huku zaidi ya nusu ya watu (milioni 20.6) wakihesabiwa katika eneo hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live