Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU kuchunguza manunuzi Dawa na Vifaa Tiba Morogoro

Ea1d471b71fbac651b2d61b87c111b3c.jpeg TAKUKURU kuchunguza manunuzi Dawa na Vifaa Tiba Morogoro

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro inatarajia kuanzakufanya uchunguzi kuhusiana na ununuzi, usambazaji wa dawa na vifaa tiba katika Zahanati ,Vituo vya Afya na Hospitali zilizopo mkoani humo.

Lengo la uchunguzi huo ni kubaini endapo kuna vitendo ama viashiria vya rushwa ili kuchukua hatua stahiki dhidi ya wale watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo ziweze kuchukuliwa.

Mkuu wa Takukuru mkoa huo , Manyama Tungaraza amesema, hayo Julai 29, 2021 katika taarifa yake kwa umma kupitia vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Aprili hadi Juni 2021.

Licha ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi hiyo amesema, kuanzia Julai hadi Septemba 2021 ,Takukuru imeweka vipaumbele vitatu ambapo ni pamoja na kufanya uchunguzi kuhusiana na ununuzi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba.

Pia itaendelea na uchunguzi wa tuhuma zote zinazohusiana na migogoro ya ardhi hususani urasimishaji ardhi ambao unalalamikiwa na wananchi wengi katika wilaya za mkoani humo.

Ametaja kipaumeble kingine ni kutoa elimu ya rushwa na madhara yake kwa jamii katika mikutano ya hadhara kupitia mpango wa Takukuru inayotembea na semina.

Mkuu wa Takukuru mkoa amesema ,Taasisi hiyo itaendelea kuimalisha klabu za Wapinga Rushwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo kama njia ya kuwajengea uwezo wanafunzi ili wawe waadilifu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz