Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAFITI: Wasiooa hufa zaidi kwa magonjwa ya moyo

A Man Having A Heart Attack.png Tafiti zimebaini watu wasiooa ama kuolewa wapo hatarini kuugua Magonjwa ya Moyo

Thu, 2 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti umeeleza kwamba watu ambao hawajaoa ama kuolewa wapo kwenye hatari zaidi ya kufariki dunia kwa magonjwa ya moyo, na kwamba hata ule uwezo wao katika kujisimamia huwa ni mdogo ukilinganisha na watu waliooa ama kuolewa.

Dk Fabian Kerwagen wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Wurzburg Ujerumani amesema kwamba watu waliooa ama kuolewa wanayonafasi kubwa ya kuishi kutokana na usaidizi wanaoupata kutoka kwa wenzi wao ikiwemo kukumbushwa suala la utumiaji wa dawa kwa wakati.

"Tumegundua kwamba wagonjwa ambao hawajaolewa ama kuoa wanashindwa kuhusiana na jamii ukilinganisha na waliooa ama kuolewa na pia wanakosa uthubutu wa namna ya kukabiliana na magonjwa hayo, bado tunachunguza," amesema Dkt. Kerwagen

Aidha Dkt. Kerwagen amewasisitiza wahudumu wa afya kuwauliza wagonjwa wenye matatizo ya moyo kuhusu hali zao za mahusiano na wahakikishe wanawahamasisha ili wawe na uwezo wa kujisimamia wenyewe.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live