Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TACAIDS yahimiza wadau kuja na mawazo bunifu ya kutokomeza unyanyapaa

Stigy Mbinu mbadala zinahitajika

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wa masuala ya UKIMWI wametakiwa kuandaa mkakati wenye tija ili kuondoa unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU hatua itakayosaidia kufikia malengo ya kitaifa na kidunia ya kumaliza unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha kupitia mkakati wa kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi katika Mwitikio wa UKIMWI, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko amesema ubaguzi na unyanyapaa ni moja ya malengo ya kidunia ifikapo 2030 kusiwe unyanyapaa kwa mtu anayeishi na VVU.

Amesema shughuli kubwa ya kikao hicho ilikuwa ni kuhuisha Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi kwa WAVIU ambao sasa umepitwa na wakati, na kwamba kutokana na mambo mapya yanayojitokeza, mkakati huo uliopo ni wa mwaka 2013-2017 hivyo wanahitaji kutengeneza mkakati mpya unaoendana na wakati wa sasa na yale mazuri yaendelezwe.

“Upatikanaji wa mkakati wenye kuleta matokeo sahihi utatokana na mawazo pamoja na michango ya wadau watakaoshiriki katika kuandaa mkakati huu ambapo pia itasaidia wataalam elekezi kuja na mkakati wenye mawazo yenu.

“Huwezi kufanikisha jambo bila mkakati, hivyo mjione mnakazi kubwa ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mnaweka mawazo yenu vizuri kwenye mkakati huu ili kufikia malengo, mawazo yenu pia yatasaidia kuja na mkakati wenye mawazo yetu wenyewe ambao utakuwa rahisi kutekelezeka na kupata matokeo chanya,” amesema Dk. Maboko.

Ameongeza kuwa takwimu za mwaka 2021 kwenye ubaguzi wanje inaonekena mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa asilimia 19.5, kwa ubaguzi na unyanyapaa, ukifuatiwa na Tanga asilimia 10.5.

“Upatikanaji wa mkakati huu utasaidia kutuongoza ni mikoa gani tuanze nayo utekelezaji, ubaguzi wa ndani ambao ni asilimia 6.4 ambapo mkoa wa Geita ni asilimia 27, Mtwara asilimia 26.6 na Tanga asilimia 17, kwa kutumia takwimu hizi zitatusaidia kuona wapi tuanzie katika utekelezaji wa mkakati huu baada ya kukamilika,” amesema Dk. Maboko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live