Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TACAIDS kuja na mbinu mpya kukabiliana na UKIMWI

HIVandAIDSbasics TACAIDS kuja na mbinu mpya kukabiliana na UKIMWI

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), imefanya kikao cha Kamati ya utekelezaji wa Programu ya Mwitikio wa UKIMWI nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 17, 2022 jijini Dodoma kwa kushirikisha Menejimenti ya TACAIDS ambapo Mwendeshaji wa kikao hicho ni Kamisheni ya Tume hiyo.

Lengo la Kikao hicho ilikuwa ni kufanya ufuatiliaji wa shughuli zinazotekelezwa na TACAIDS kuona kama zimetekelezwa kwa malengo yaliyokusudiwa kwenye Sheria ya Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania Na. 22 ya mwaka 2001 na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 2015 na kuwafikia walengwa kama ilivyotarajiwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Programu, Sheikh Khamis Mataka, amesema vikao hivyo ni moja ya ufatiliaji wao kama viongozi wa Tume kufahamu kwa kina namna shughuli zinavyotekelezeka kuendana na mipango iliyopangwa na Tume.

“Vikao hivi kwetu ni muhimu sana kwani huwa tunashiriki wakati wa upangaji kabla bajeti haijapelekwa Bungeni na baada ya kurejea huwa kuna utekelezaji ambao hufanywa na wataalamu wetu, kabla ya kukaa kikao kikubwa cha kamisheni tunakaa kwanza na wataalamu wanatupatia utekelezaji wa mipango yao na kuona kama imeendana na makubaliano tuliyoyaweka awali,”alisema Sheikh Mataka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live