Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TACAIDS: Maambukizi ya virusi vya UKIMWI yamepungua

HIVAIDS Ribbon 1600x900.png TACAIDS: Maambukizi ya virusi vya UKIMWI yamepungua

Sat, 17 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imesema maambukizo ya Virusi vya Ukimwi Tanzania yameendelea kupungua hadi kufikia wagonjwa 54,000 kwa Mwaka 2021 kutoka 81,000 Mwaka 2017.

Akitaja moja ya sababu ya kupungua kwa maambukizi, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume TACAIDS, Dkt. Hedwiga Swai amesema ni matumizi ya dawa za kujikinga na HIV ambazo zinatumika kabla ya tendo la ndoa ili kujikinga na maambukizi na zipo ambazo zinatumika baada ya tendo.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko amesema idadi ya vifo pia imepungua kutoka 32,000 kwa mwaka hadi 29,000 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live