Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumbawanga wahimizwa tahadhari kuepuka magonjwa

De936aabcead4b4ffbfbe1d608077860 Sumbawanga wahimizwa tahadhari kuepuka magonjwa

Sun, 21 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya (DC) ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Dk Halfan Haule, amewataka wakazi katika Mji wa Sumbawanga na vitongoji vyake kuchukua tahadhari kwa kuzingatia usafi na maelekezo ya wataalamu ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa yakiwamo yanayoambukizwa kwa njia ya hewa.

Alisema hayo mwishoni mwa juma wakati akitoa salamu za serikali katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga kilichojadili na kupitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya Manispaa hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

“Unaona hapa hatutumii wala kushirikiana kipaza sauti kimoja, kwa kuwa tunachukua tahadhari, hivyo tukae kwa kupeana nafasi …” alisema.

Mkuu wa wilaya huyo aliwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni zote za afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji tiririka.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Boniface Kasululu, alisema kwa simu kuwa, wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari zote muhimu dhidi ya maambukizo ya magonjwa ya kuambukiza hasa kwa njia ya hewa.

“Wote tunapaswa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuzingatia kanuni zote za usafi ikiwa pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka na kutumia tiba za asili kama Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto inavyoelekeza," alisema Dk Kasululu.

Aliwahimiza wananchi kuepuka kuishi kwa hofu, badala yake wanapoona dalili za ugonjwa wowote, wafike kwa wataalamu kupata huduma za afya na kwa matibabu kwa wakati.

Chanzo: habarileo.co.tz