Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika Ndugai leo anazindua zoezi la kupima VVU kwa Wabunge

9693 P1 TZWeb

Thu, 21 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo anazindua zoezi la kupima Ukimwi kwa Wabunge kwa hiari.



Akizungumza leo, Juni 21, 2018 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na Majibu, Naibu Spika, Tulia Ackson amesema ni vizuri wabunge wote ambao hawajapimwa wakapime Virusi Vya Ukimwi kwa hiari.

“Waheshimu wabunge leo Mh. Spika anatarajiwa kuzindua zoezi la kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari hapa Bungeni kwa waheshimiwa Wabunge lakini pia na wafanyakazi wa Bunge na atazindua zoezi hilo saa nne leo hii kwenye viwanja vya vilivyopo nyuma ya ukumbi wa Mh. Pius Msekwa,” amesema Dkt. Tulia Ackson.

“Kwahiyo Waheshimiwa Wabunge hasa wale wenye Kamati ya Ukimwi mnaombwa kuhudhuria zoezi la uzinduzi alafu waheshimiwa Wabunge wale wote ambao hawajapima wanaomba kuanzia saa 7 waende kupimwa kwa hiari ili wabunge tuwe tunafahamu afya zetu vizuri.”

Loading...
Chanzo: bongo5.com