Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siri ya kuishi maisha marefu na ugonjwa wa BP hii hapa

58701 Pic+shinikizo

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Watu wanaosumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu (BP) wanaweza kuishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu endapo watazingatia masharti ya daktari.

Akizungumza na Mwananchi jijini hapa jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dk Wilfred Rutahoile alisema kuna aina mbili ya shinikizo la damu, linalotokea bila kuwa na chanzo cha ugonjwa na lile linalosababishwa na ugonjwa mwingine.

“Shinikizo la damu haliponyeki kama chanzo chake hakijulikani na mgonjwa atakaa nalo muda mrefu hivyo anatakiwa kuli-control (kulidhibiti) kila siku ya maisha yake mpaka siku atakapoondoka duniani.”

“Tatizo hilo linajijenga kidogo kidogo kwa takribani hata miaka 10 kabla mgonjwa hajapata madhara kwani halina dalili, lakini akiwa na mafuta mengi mwilini msongo wa mawazo, kutumia chumvi kupita kiasi, pamoja na mambo mengine presha inaweza kuongezeka,” alisema.

Hata hivyo, Dk Rutahoile alisema ili kudhibiti ugonjwa huo na kuishi maisha marefu, inatakiwa kujenga tabia ya kupima mara kawa mara na kutumia dawa pindi mtu anapogundulika kuwa nao.

“Mtu anaweza kwenda hospitali na kuambiwa ana tatizo hilo, basi anaanza kusema nilianguka jana nikawa na tatizo hilo ama niligombana na mtu jana, hivyo havina uhusiano ni vizuri kuonana na wataalamu wa magonjwa hayo ili kupata ushauri,” alisema.

Pia Soma

Dk Rutahoile alisema ili kuzuia ugonjwa huo pia inatakiwa kupunguza matumizi ya chumvi, pombe, kupunguza unene na kufanya mazoezi mengi.

Akizungumzia ugonjwa huo, mkazi wa Dodoma Mjini, Saidi Mohamed aliwataka wananchi kufanya mazoezi kwa wingi ili kuufanya mwili kuwa na uzito unaotakiwa kitaalamu hivyo kuepuka ugonjwa huo.

“Ninavyofahamu unapofanya mazoezi unaondoa mafuta yasiyohitajika mwilini ambayo muda fulani yakiwa mengi yanaganda kwenye mishipa ya moyo na kufanya mapigo ya moyo kutokuwa sawa, hivyo wananchi wanatakiwa kufuafa masharti ya daktari ili kuepukana nao na wale walionao waweze kujua jinsi ya kuudhibiti,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz