Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio kila panapouzwa dawa ni 'Pharmacy'

Pharmacy Ses Sio kila panapouzwa dawa ni 'Pharmacy'

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania, Fadhili Hezekiah amesema kuwa muingiliano wa kimaslahi na uelewa mdogo wa Masuala ya ufamasia, ni miongoni mwa vyanzo vinavyopelekea uvunjifu wa kanuni na sheria kwenye maduka ya dawa muhimu nchini, kwakuwa asilimia kubwa ya wamiliki wa maduka hayo si wafamasia, bali ni wataalam wenye taaluma zingine katika kada ya afya na kuwa sio kila panapouzwa dawa ni pharmacy.

Hezekiah amebainisha hilo kwenye mahojiano maalum na Wasafi Media kupitia ripota wetu @hamisimguta muda mfupi baada ya kumalizika kwa Kongamano la nane Wanafunzi wa Famasia katika chuo cha Elimu ya Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha kuibuka kwa tabia za uvunjifu wa sheria na kanuni kwenye maduka hayo.

"Maduka ya dawa yapo ambayo ni 'Pharmacy' na yapo ambayo ni maduka ya dawa muhimu, sasa namna ya uwasilishaji wa taarifa mara nyingi watu huchukulia popote panapouzwa dawa ni pharmacy, pharmacy ni eneo ambalo kunatolewa huduma za dawa na kuna mtu mwenye shahada ya ufamasia ambaye ndio mfamasia, tofauti na hapo inageuka kuwa duka la dawa muhimu... huduma zote zitakazotolewa hazihusu uchunguzi na masuala ya kitabibu, ikitokea imefanyika hivyo ni makosa kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live