Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simulizi ya mgonjwa wa Corona

Covid 19 Simulizi ya mgonjwa wa Corona

Mon, 12 Jul 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwanadada Neema mkazi wa Dar es Salaam, ametoa simulizi yake namna alivyoanza kuumwa kifua, mafua na mwili kuishiwa nguvu katika wimbi hili la tatu la maambukizi ya Virusi vya Corona hadi baadaye alipokuja kugundulika na ugonjwa huo.

Submitted by Agnes Kibona on Jumatatu , 12th Jul , 2021 Kipimo cha COVID-19

Akizungumza huku akitoa sauti kwa shida kidogo hii leo Julai 12, 2021, kupitia kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, Neema amesema kuwa dalili za awali alizozipata alihisi pengine ni mzio (Allergy) ama vumbi na akaanza kunywa chai yenye limao ndani yake.

"Baadaye nikaanza kutumia dawa kwa ajili ya kifua, nikaamua kwenda hospitali nikafanyiwa vipimo na muda huo mwili ukaanza kuchoka, nikapimwa kila kitu nikaambiwa nina UTI na nikapewa antibiotic lakini baada ya kurudi nyumbani nikawa napata homa kali," amesimulia Neema

Sehemu ya pili ya simulizi hii ya Neema itaendelea kesho kwenye kipindi cha SupaBreakfast kinachoanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi.

Chanzo: eatv.tv