Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku za hedhi kikwazo kwa wasichana kusonga kielimu

21536e860516380a6df038947063e8cf Siku za hedhi kikwazo kwa wasichana kusonga kielimu

Sun, 22 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ASILIMIA 15 ya wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria shule katika siku zao za hedhi.

Aidha zaidi ya asilimia 42 ya wasichana wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya hedhi na 34 asilimia wakishindwa kuhudhuria masomo kwa hofu ya kujichafua kwa sababu ya kukosa kitu sahihi cha kujistiri.

Hayo yote yamebainishwa katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu NIMR katika wilaya 14 za Tanzania Bara

Katika utafiti huo pia imebainishwa kuwa asilimia 26 ya shule hazina miundombinu rafiki wakati kwa msichana wakati akiwa kwenye kipindi cha siku zake.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya taulo za kike zilizotolewa na Benki ya CRDB, kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kaskazini Chiku Issa alisema kwamba wametoa msaada huo kupitia kampeni maalumu ya Hedhi Salama kwa Elimu Bora.

Msaada huo uliolenga shule ya Sekondari Old Tanga ya Jijini Tanga ili kuwasaidia watoto wa kike kusoma kwenye mazingira salama una thamani ya Sh milioni 5.

Meneja huyo wa CRDB alisema kwamba wao kama benki wanaamini upatikanaji wa taulo za kike ni muhimu kwa mahudhurio ya mtoto wa kike shuleni na kupata haki yake ya msingi ya elimu .

Kwa upande Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari aliwashukuru Benki ya CRDB kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia katika kuboresha masomo kwa kupunguza changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kujistiri kwa wasichana hao wanapokuwapo shuleni.

Chanzo: habarileo.co.tz