Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku ya Kinamama Duniani Hospitali ya Mwanayamala yapokea msaada wa vifaa tiba

77F6B7CF F52F 42EC B9C0 335769E7726E 660x400.jpeg Siku ya Kinamama Duniani Hospitali ya Mwanayamala yapokea msaada wa vifaa tiba

Mon, 10 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Boomplay ni inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki imeadhimisha Siku ya kina mama mwaka huu kwa kutoa vifaa vya matibabu kwa Hospitali ya Mwananyamala, kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo za afya salama na uhakika kwa akina mama nchini.

Hospitali hiyo, ambayo ni hospitali Kuu ya Rufaa jijini Dar es Salaam inahudumia wastani wa akina mama wajawazito 900-1,400 kila mwezi.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la hospitali siku ya Jumapili, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mipango endelevu inayolenga kusaidia jamii.

“Tunayo furaha kutumikia jamii yetu na hasa katika siku hii ya akina Mama duniani. Tunaelewa mchango na shida wanazopitia akina mama hasa wakati wa uzazi katika jamii zetu” 



Tunapowasherehekea kina mama, tunafurahi kuchangia msaada wetu na tunatarajia kufanya mengi zaidi kwenye jamii katika siku usoni, “>>>> Stambuli

Hamasa hiyo iliungwa mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Zavery Benela, ambaye aliisifu Kampuni hiyo kwa msaada wake, na kuongeza kuwa umekuja katika muda muafaka wakati ambao Ulimwengu unakabiliwa na changamoto ya huduma ya afya.



“Kwa niaba ya hospitali nzima, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Boomplay kwa msaada huu wa huruma. Tuna hakika kuwa mchango wao utasaidia sana katika kuhakikisha huduma zetu za kina mama zinaendelea bila kukatizwa,”>>>> Dr. Zavery Benela.

“Ninahimiza Kampuni na wadau wengine kuiga ishara hii nzuri, ili kutimiza juhudi zetu katika kuhakikisha kuwa akina mama na watoto wao wachanga wanapata huduma na matibabu ya hali ya juu”
Chanzo: millardayo.com