Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule 20 kupatiwa elimu ya ukimwi Kwimba

HIV6Shule 20 kupatiwa elimu ya ukimwi Kwimba

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MRATIBU wa Mradi wa Elimu ya Ukimwi kwa Vijana, Sebastian Gregory amesema wapo katika mpango wa kutoa mafunzo ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa shule 20 za sekondari wilayani Kwimba.

Alisema hayo wakati wa mafunzo maalumu ya VVU kwa walimu wa shule za sekondari katika kata ya Sumve wilayani humo juzi.

Gregory alisema kupitia mradi huo watatembelea shule za sekondari Mushialage, Sumve, Nyamikoma, Mantare, Ishingisha na Bumengeja, ambapo pamoja na kutoa elimu hiyo, piawanafunzi watafanyiwa vipimo vya VVU.

Aliwataka watoa huduma wa vituo vya afya kuepuka kutumia lugha zisizokuwa nzuri kwa wanafunzi walioathirika na virusi vya ukimwi.

Mradi huo wa elimu ya ukimwi kwa vijana unadhaminiwa na Ambassador's Fund for HIV/AIDS relief.

Daktari kutoka Hospitali Teule Sumve, Dk Abdallah Bihoga alisema kwa takwimu za mwaka 2019 katika kata ya Sumve kuna watoto 114 wanaendelea na dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (ARVs) kati yao wapo wa umri wa miaka 0 hadi 14 na wa umri wa miaka 15 hadi 19.

Alisema mwitikio wa vijana kwenye kliniki ya watu waliotharika na VVU ni mkubwa kutokana na kuwekewa siku za mwisho wa wiki kuhudhuria kliniki.

Hata hivyo, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bungulwa, Godfrey Mahimbo alisema uelewa wa walimu wengi wa jinsi ya kuishi na vijana waliothirika na VVU bado ni mdogo.

Alisema kuna wakati walimu hutoa adhabu kwa wanafunzi wote shuleni bila kujali kuwa wengine ni waathirika wa virusi hivyo.

Chanzo: habarileo.co.tz