UVUTAJI wa Shisha umeelezwa kupunguza nguvu za kiume, magonjwa ya Moyo, Figo, Kifua, Saratani ya Koo na Mapafu pamoja na Corona.
Hayo yamesemwa leo Novemba 10,2021 Mjini Morogoro na Kamishna Msaidizi wa Kinga na Huduma za Jamii, kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Moza Makumbuli katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wandishi wa vyombo mbali mbali vya Habari nchini.
Amesema uvutaji wa Shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara 100 hadi 200. Aidha akifafanua madhara ya Shisha amesema uvutaji shisha hautoi moshi ule kama wa tumbaku bali utoa mvuke ambao uchanganywa na fleva mbali mbali ikiwemo ya Vanilla, Strawbery na kahalika ambapo watu wasio waamifu uchanganya tumbaku pamoja na bangi na madawa ya kulevya na upelekea watumiaji kutumbukia kwenye urahibu wa madawa ya kulevya.
Amesema madhara mengine ya utumiaji Shisha mtumiaji anajjiweka kwenye hatari ya kupata kansa ya koo na mapafu kutokana na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiajji awe kwwenye hatari kubwa ya kupata matatizo hayo.
Pia Shisha imetajwa kusababisha magonjjwa ya moyo kutokana na moshi wa tumbuku ambao husababisha mishipa ya damu ya artery kuziba na matokeo yake moyo unashindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Madhara mengine yaliyobainika ni Maambukizi ya ugonjjwa wa Kifua Kikuu, Corona na Fangasi kutokana na kupokezana bomba la kuvutia shisha.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DCEA, Florence Khambi amesema utamaduni wa Shisha umeigwa kutoka njje na kwamba Shisha ipo kwenye jamii ya tumbaku ambayo haipo chini ya Mamlaka yao.
“Tumbaku sio misheni ya mamlaka, inaingizia kipato taifa, ila mwaka 2013 tulibaini watumiaji wa shisha wanapovuta wanalewa, tulishirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ikapigwa marufuku lakini kwa sasa ile katazo limelega lega na imeibuka tena kwa wingi mno ni vema mamlaka kushirikiana na kutoa elimu zaidi ya madhara ya shisha kwa jamii.
“Shisha imekuwa mlango wa kutumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya, wauzaji wa madawa wana mbinu nyingi ya kupata soko la kuuza dawa zao,”amesema.