Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika laanzisha programu ya afya ya uzazi kwa vijana

315e43e75441b014b6581d90c880a945.png Shirika laanzisha programu ya afya ya uzazi kwa vijana

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Mwanza Children Youth Network (MCYN) limeanzisha programu maalum ya afya ya uzazi pamoja na uzazi wa mpango kwa vijana ili kuwaepusha na mimba za utotoni na magonjwa ya zinaa.

Hayo yamesemwa na Ofisa Uelimishaji wa shirika hilo, Agnes Marco.

Alisema wameamua kutoa elimu hiyo ili kunusuru kundi kubwa la vijana wanaokosa huduma hiyo kutoka kwa wazazi wao.

"Tunajua teknolojia ilivyo kwa sasa na kundi hili la vijana ndio hatari zaidi kutumbukia kwenye mimba za utotoni kutokana na wazazi au walezi kushindwa kutoa elimu hiyo kwa kigezo cha tamaduni za Kiafrika," alisema.

Alisema mradi huo utanufaisha vijana zaidi ya 170 kutoka wilaya ya Ilemela. Marco alisema mradi huo umeanza mwezi huu na unatarajiwa kumalizika Juni, mwakani.

“Elimu hiyo itawapa ufahamu vijana juu ya njia sahihi za matumizi ya njia salama za uzazi wa mpango kama vijiti, vitanzi, sindano pamoja na kalenda,” alisema.

Aliwataka wazazi kutokwepa jukumu la kuwafundisha watoto wao elimu ya afya ya uzazi ili wasiweze kuangamia na kuwa wategemezi.

Kwa upande wake, Mwalimu wa Afya ya Vijana, Swaumu Majala alisema vijana wengi wana uelewa mdogo wa afya ya uzazi. Alitoa wito kwa waelimishaji rika, serikali na wadau wa afya kuongeza kasi ya kuwafikia vijana wengi na kuwapatia elimu hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz