Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shinyanga Yakanusha Kuzidiwa na Wagonjwa wa Corona

SHY WEB?fit=700%2C400&ssl=1 Shinyanga Yakanusha Kuzidiwa na Wagonjwa wa Corona

Tue, 13 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Shinyanga Yakanusha Kuzidiwa na Wagonjwa wa Corona July 13, 2021 by Global Publishers



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati, amekanusha uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa mkoa huo ume zidiwa na wagonjwa wa COVID-19 na una upungufu wa mitungi ya Oksijeni na kuitaka jamii kuupuuza uzushi huo.

Akizungumza na watumishi wa umma, Mkuu wa mkoa huo amesema kuwa watachukua hatua kali kwa mtu aliyehusika kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuwa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga imeelemewa na wagonjwa wa COVID-19.

Aidha RC Sengati akatumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz