Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh7 bilioni kutumika ujenzi kituo cha magonjwa ya mlipuko Tanzania

101914 Kituo+pic Sh7 bilioni kutumika ujenzi kituo cha magonjwa ya mlipuko Tanzania

Fri, 10 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania itatumia Sh7 bilioni kujenga kituo maalumu cha kutolea huduma ya magonjwa ya mlipuko kitakachokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 200.

Kituo hicho kitajengwa katika eneo la Kisoka kilomita moja kutoka ilipo hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na makatibu wakuu 14 na wajumbe wa kamati ya kitaifa ya kupambana na virusi vya corona, meneja mradi wa ujenzi wa kituo hicho Kanali Solomoni Shaushi amesema baadhi ya majengo yatakamilika  Aprili 30, 2020.

Amesema ujenzi huo unafanywa na kikosi cha ujenzi cha Suma JKT na tayari jeshi limeshapeleka nguvu kazi ya wanajeshi 389 kukamilisha ujenzi wa majengo yote baada ya miezi sita.

Katibu mkuu Wizara ya Afya, Dk Zainabu Chaula amesema kituo hicho kitakapokamilika kitatumika kuweka wagonjwa na washukiwa wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo corona.

“Serikali imeamua kujenga kituo hicho kitakachogharimu Sh7 bilioni na kitakapokamilika kitakuwa cha aina yake nchini kwani kitaweka vifaa vya kisasa vya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa magonjwa ya mlipuko,” amesema Dk Chaula.

Pia Soma

Advertisement
Katika hatua nyingine makatibu wakuu wakongozwa na katibu mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Uweklezaji Doroth Mwaluko wamefanya ziara katika hosteli za Magufuli zinazoweka karantini wasafiri walioingia jijini Dar es Salaam wakitokea nje ya nchi, kituo cha matibabu kwa wagonjwa wa corona kilichopo Kibaha na kituo cha muda kilichopo Kisoka Mloganzila.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Dk Rashid Mfaume amesema hadi jana Aprili 8, idadi wasafiri walioingia jijini Dar es Salaam wakitokea nje ya nchi na kukaa karantini katika hosteli za Magufuli wamefika 226 na kati yao 72 wameruhusiwa kutoka baada ya kukamilisha siku 14 za uangalizi na kwamba kituo kimebaki na wasafiri 154.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz