Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh284bilioni zatumika kujenga, kuboresha vituo vya afya Tanzania

54810 Pic+afya

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo amesema Rais John Magufuli ametoa Sh284.5 bilioni kwa ajili ya kuboresha na kujenga vituo vipya vya afya nchini.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 30 katika viwanja vya Mwakangale wilayani Kyela katika ziara ya Rais Magufuli mkoani Mbeya.

“Tukizungumzia sekta ya afya juzi  tu kule Mbonde Mtwara Rais umezindua kituo cha afya kikiwa ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyoboreshwa 352, vituo vya afya vipya 67 ambavyo vimetumia Sh284.5 bilioni.”

“Tunakushukuru ndiyo maana watu wa Ipinga wanafahamu kituo chao cha afya ni bora kuliko hospitali ya wilaya, tumeshaleta dawa, vifaa tiba na vifaa vya kisasa mpaka pasi pale ipo,” amesema Jafo.

Aidha, Jafo amesema Rais ameidhinisha Sh52.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa shule, madarasa, nyumba za walimu na vyoo.



Chanzo: mwananchi.co.tz