Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh bilioni 6 kusaidia watoto njiti nchini

Njiti Picfvb Sh bilioni 6 kusaidia watoto njiti nchini

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imetoa Sh bilioni 6.3 kwa ajili ya kununua vifaa tiba nchi nzima. Vitaa hivyo vitasaidia watoto wachanga na waliozaliwa kabla ya muda (njiti) kupata afya bora.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa mkoani Shinyanga, amesema vifaa vitakavyokabidhiwa vina thamani ya Sh milioni 170 katika wodi ya watoto mahututi.

Ummy amekabidhi vifaa tiba kwenye Hospitali ya Rufaa na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya, Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Christina Mdeme.

Waziri Ummy alisema amefarijika kuona huduma za afya zinatolewa vizuri kwa wagonjwa na Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma bora za afya, pamoja na kuokoa afya za watoto wachanga na njiti.

“Vifaa hivi vitapelekwa pia katika Hospitali ya Kahama na Kishapu, Rais Samia anataka kila Mama Mjamzito aondoke na kichanga chake kiikiwa salama ndiyo maana akatoa vifaa tiba,”alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliwataka wakurugenzi kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kuajiri watumishi wa afya ili wananchi wapate huduma.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi alishukuru kupokea kwa vifaa huku akiwahidi yote yaliyo elezwa watayasimamia na kutekeleza ipasavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live