Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawekeza Sh6.7 trilioni sekta ya afya

Sindano Vifoooo Serikali yawekeza Sh6.7 trilioni sekta ya afya

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini ili kuhakikisha afya za wananchi zinaimarika

Dk. Mollel amebainisha hayo wakati alipo mwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uzinduzi wa Chuo cha Afya Litembo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Dk. Mollel amesema kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi ya Trilioni 6.7 katika sekta ya afya ili kuboresha miundombinu, upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendaanishi, kuongeza watumishi wa afya pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wataalamu wa afya kupitia programu ya Samia Scholar ship ndani ya miaka miwili katika sekta ya afya .

“Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Dk. Samia amewekeza zaidi ya Bilioni 4 ili kuhakikisha wananchi wa Mbinga wanapata Huduma bora za afya ili kuwa na afya bora na kuendelea na maisha yautafutaji ili kujenga nchini”, ameeleza Dk. Mollel

Aidha katika kwendelea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi pamoja na Taasisi za Dini, Rais Samia amekuwa ni kiunganishi ili kuhakikisha sekta binafsi wanafanya vizuri nchini.

Ameongeza kuwa Serikali ndani ya mwaka huu 2023 imenunua magari ya kubeba wagonjwa 727 na magari 201 yameshafika ndani ya nchini na hivi karibuni yatazinduliwa na kusambazwa katika maeneo yenye uhitaji wa magari ya kubeba wagonjwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo amesema chuo hicho kitakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma na jirani kwani watazalisha wataalamu mbalimbalai wa sekta ya afya na kusaidia kuhudumu katika vituo vya kutolea Huduma za afya nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live