Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa tahadhari ugonjwa wa manjano

Manjano Serikali yatoa tahadhari ugonjwa wa manjano

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa homa ya manjano (yellow fever), ambapo amesema Machi 3, mwaka huu, Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO, ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini Kenya.

Hata hivyo amesema hakuna taarifa yoyote ya kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, hadi kufikia Machi 3, mwaka huu nchini Kenya kulikua na wagonjwa wa homa ya manjano 15 na vifo vitatu.

Amesema katika sampuli sita zilizopimwa maabara ya Kenya kwa kutumia vipimo vya serology na PCR, sampuli tatu zilithibitika kuwa na maambukizi.

“Hapa nchini taarifa ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita katika mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa, zinaonesha hakuna taarifa zinazoashiria kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya manjano, pia taarifa za ufuatiliaji wa tetesi za magonjwa haujaashiria kuwepo kwa ugonjwa huo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live