Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa neno kuhusu ugonjwa wa Ebola

7847 IMG 9153 TZW

Sun, 13 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Serikali imesema kuwa hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitika kuwa na virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola, lakini Tanzania iko katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa watu.



Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Lakini hadi sasa hakuna mtu ambaye anahisiwa au kuthibitika kuwa na virusi vya Ebola, kutokana na kupakana na DRC, nataka kukiri kwamba tuko hatarini kuambukizwa ugonjwa huu kutokana na mwingiliano wa watu hawa wanaosafiri kutoka na kuingia Tanzania.” Ummy alisema hatari kwa Tanzania inatokana na kuwepo kwa mwingiliano mkubwa wa wafanyabaishara wanaokwenda DRC, hususani wale wanaotumia njia zisizo rasmi kwa kuvuka Ziwa Tanganyika na mitumbwi. “Napenda kutoa tahadhari kwa wananchi wote.

Ummy alitoa tahadharikwa nchi nzima hasa katika mikoa ambayo inapakana na DRC, ni mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Katavi, Rukwa na Songwe. Alisema ili kujikinga na ugonjwa wa Ebola, Wizara imeimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko katika mikoa ambayo inapakana na DRC, mipakani na viwanja vya ndege vyote nchini kwa kuweka vifaa vya kubaini joto la mtu (Themo scanner).

Waziri Ummy alisema kuwa Wizara imeimarisha mfumo wa ufuatiliaji wagonjwa katika mikoa yote, kusambaza miongozo, vifaa na imeagiza makatibu tawala wa mikoa na wakuu wa mikoa kushiriki katika kutoa taarifa inapotokea dalili zozote. “Niwatake Waganga Wakuu wa mikoa wote lakini hasa hawa ambao wanapakana DRC wasilale, wahakikishe kunakuwa na ufuatiliaji kwa wageni kwa kuweka daftari, mifumo na vifaa maalumu vya kutambua,” alisema. Ummy alisema hivi sasa kuna wodi ambayo imetengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola, watakaobainika katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke.

Loading...
Chanzo: bongo5.com