Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa hadhari wimbi jipya Covid-19

187df612c358c649be2c475e664332f3.jpeg Serikali yatoa hadhari wimbi jipya Covid-19

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imewataka wananchi wote kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) huku ikisema upo uwezekano wa kutokea wimbi la tatu la maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini.

Kadhalika,serikali imepokea mapendekezo yote 19 yaliyotolewa na Kamati maalumu iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ya kufanya tathmini ya ugonjwa wa COVID-19 na inaendelea kuyafanyia kazi na taarifa ya utekelezaji wake itatolewa hivi karibuni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Leonard Subi alisema tahadhari hiyo

imetolewa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo katika nchi za Afrika na nchi jirani na Tanzania.

“Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 katika nchi yetu,hii inatokana na ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu unaofanywa na wizara na mwingiliano wa watu wetu na watu wa mataifa jirani na pia ulimwenguni,”alisema Dk Subi.

Alisema tishio hilo pia kwa sasa linaonesha kuwakumba watu wa rika lote wakiwemo wenye umri mdogo na kutaka viongozi wote wa serikali, mikoa, wilaya, viongozi wa dini, wakuu wa taasisi za umma na binafsi kuwaelimisha wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

“Jukumu la kinga dhidi ya

ugonjwa huu ni la kila mmoja wetu,hivyo tusiwe na hofu ila tuendelee kuzingatia afua za kinga,”alisisitiza Dk Subi.

Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Juni 7 hadi 13, mwaka huu,katika Kanda ya Afrika, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imekuwa ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo na mfano ni nchi za Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Namibia, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Angola na nchi nyingine,idadi ya wagonjwa imeendelea kuongezeka bila kushuka.

Aidha alisema nchi hizo zimekumbwa na anuai ya virusi vipya ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19 kuwa mkali zaidi.

Kutokana na hayo,Dk Subi alizitaka halmashauri na maafisa afya wanoatoa huduma mipakani kuendelea kuimarisha udhibiti

wa magonjwa katika maeneo hayo kwa mujibu wa miongozo husika na kufuatilia magonjwa na matukio hatarishi kwa afya kwenye maeneo yao.

Akisisitiza hatua za kujikinga na ugonjwa huo,Dk Subi alisema uvaaji wa barakoa uendelee kwenye maeneo yote yenye msongamano wa watu, kunawa mikono mara kwa mara na maji tiririka na sabuni,kutumia vipukusi na kuepuka msongamano isiyo ya lazima.

“Tuepuke misongamano isiyo ya lazima hasa kwenye misiba,kanisani,viwanja vya michezo,usafiri na mengine na kuhakikisha eneo ulilopo lina mzunguko mzuri wa hewa,”alisema Dk Subi.

Aidha aliwataka watu wote watakaokuwa na dalili za ugonjwa huo kuwahi mapema kwenye vituo vya kutolea huduma za tiba.

Chanzo: www.habarileo.co.tz