Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa bilioni 26/- ununuzi vifaa tiba

Dfc6c3ddde87c6dbea6dc0be5b2b991f Serikali yatoa bilioni 26/- ununuzi vifaa tiba

Fri, 16 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SH bilioni 26 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyojengwa katika awamu ya kwanza na pili ya mwaka 2020/2021 na tayari Sh bilioni 15 zimepelekwa kwenye vituo hivyo.

Aidha, vifaa tiba vya Sh bilioni 11 viko kwenye utaratibu wa kupelekwa katika vituo hivyo, huku vituo vilivyojengwa katika awamu ya tatu na nne vifaa hivyo vitanunuliwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Akijibu swali la Mbunge Viti Maalumu, Esther Midimu (CCM) bungeni jana, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dugange alisema ununuzi wa vifaa tiba unafanywa na serikali kwa awamu.

Alisema katika mwaka wa fedha 2017/18, Kituo cha Afya Mwabayanda kilipatiwa Sh milioni 400 kwa ajili ya upanuzi kwa kuwa awali ilikuwa ni zahanati.

Alisema ujenzi na ukarabati umekamilika na kituo hicho kimeanza kutoa huduma za dharura za upasuaji kwa wajawazito kuanzia Oktoba, mwaka jana baada ya kupatiwa vifaa tiba kutoka kwenye vituo vingine vilivyopo mkoa wa Simiyu.

“Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye baadhi ya vituo vya afya vilivyojengwa na kukarabatiwa ambavyo havikupewa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo,” alisema.

Dk Dugange alitoa ushauri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kupitia mapato yake ya ndani kutoa kipaumbele cha ununuzi wa vifaa tiba kwa awamu ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wakati serikali ikiendelea kutafuta fedha za ununuzi wa vifaa hivyo.

Alisema kwa kuwa zahanati hiyo imejengwa katika awamu ya nne, itapatiwa fedha mwaka ujao wa fedha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz