Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatenga bilioni 6 maboresho sekta ya Afya

Mwanza Maboresho sekta ya Afya

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima, amesema kuwa, Serikali imetenga Bilioni sita, kwa ajili ya maboresho ya huduma ya afya, katika mwaka wa fedha wa 2021 – 2022, zilizoelekezwa kukamilisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto, katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekotoure.

Dkt. Gwajima ameeleza mpango huo wa serikali Jijini Mwanza, baada ya kukagua ujenzi wa jengo la mama na mtoto, ambalo kwa sasa limefikiaa silimia 83.

Mradi huo unalenga kuboresha utoaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto, ikiwa ni pamoja na kuhudumia wakazi wa Wilaya zote saba za Mkoani humo pamoja na mikoa jirani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live