Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatenga Sh.bilioni 8 kusomesha wataalamu wa afya nje

Pesa Fedhaddd Serikali yatenga Sh.bilioni 8 kusomesha wataalamu wa afya nje

Mon, 4 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wizara ya afya imetenga Tsh. Bilioni 8 kusomesha Wataalamu wa Afya, ndani na nje ya nchi, katika fani mbalimbali za kibingwa ikiwemo upasuaji wa Watoto.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi mara baada ya kuwajulia hali watoto mapacha (Rehema na Neema) waliokuwa wameungana na kufanikiwa kutengenishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mnamo Julai Mosi mwaka huu.

Prof. Makubi amesema kuwa fedha hizo zitawasaidia wataalamu wa afya ili kuweza kujiendeleza kwa ngazi ya kibingwa na ubingwa bobezi na kuwataka Watalaamu kujitokeza.

Kwa upande wa Watoto mapacha waliofanyiwa upasuaji wa kuwatengenisha Prof. Makubi amesema upasuaji huo wa kihistoria kwa watoto hao walioungana tumbo na kifua ni mfumo bora uliowekwa na Rais Samia wa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya kwa ngazi zote nchini “Rais Samia na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wanatoa pongezi kwa Wataaalamu wetu nchini wakishirikiana na wale wa chuo Kikuu cha Bahrain kwa kufanikisha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live