Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapokea dozi za 376,320 Moderna

Chanjoopicc Data Serikali yapokea dozi za 376,320 Moderna

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko19 yakiendelea na uhamasishaji wa chanjo ukipamba moto, kwa mara ya kwanza Tanzania imepokea chanjo aina ya Moderna kwa kiasi ambacho kitatosha kuchanja watu 188,160.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya leo Desemba 24, imesema dozi hizo za Moderna zipatazo 376,320 zilizpokelewa jijini hapa, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Covax.

Imeongeza kuwa Serikali pia ilitoa ombi kwa wadau wengine wote wenye nia ya kusaidia eneo hili kwa namna moja au nyingine.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wengine wote wenye nia ya kusaidia eneo hili kwa namna moja au nyingine kujitokeza na kufuata utaratibu wa mwongozo wa serikali kuhusu suala la kuwezesha msaada huo,” amesema Waziri wa afya DK Doroth Gwajima akizungumza kuhusu ujio wa dozi hizo.

Dk Gwajima amesema dunia ni ya watu wote na kila mmoja analo jukumu la kuilinda kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Dk Gwajima amesema mapokezi ya chanjo hizo yanafanya jumla ya chanjo za Uviko 19 zilizopokelewa kufikia 6,408,950 zikijumuisha (Sinopharm, Janssen na Pfizer), ambazo zinatosha kuchanja jumla ya watanzania 3,204,475.

Amesema shukrani ni kwa wadau wetu wa Maendeleo hususani katika kujali afya za Watanzania husani mpango wa Covax ukiongozwa na mashirika ya GAVI, WHO, na UNICEF ambao wamefanikisha hilo.

Asema hivi karibuni Wizara hiyo ilitoa mwongozo wa chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania. 

“Serikali itaendelea kutoa Chanjo dhidi ya Uviko-19 katika vituo mbalimbali vya afya hapa nchini kwa mujibu wa miongozo iliyopo, hivyo niwaombe wanaohusika na zoezi hilo kuwajibika kwa kasi kubwa ili kuwawezesha watanzania wengi kupata chanjo mapema iwezekanavyo,” amesema.

Katika hatua nyingine Dk Gwajima amewaagiza Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanahimizwa kwenda kwenye vituo vya huduma za afya ili wakapate elimu kuhusu umuhimu wa chanjo na kisha kuchanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live