Serikali imepokea jumla ya dozi 576,558 za chanjo dhidi ya Corona aina ya Sinopharm kutoka China .
Haya yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa mapema Oktoba 8, 2021 jijini Dar es Salaam, na kubainisha kuwa dozi hizo zimeletwa chini ya mpango wa Shirika la Afya Duniani WHO uitwao Covax Facility.
Aidha amesema kuwa dozi hizo ni sehemu ya dozi milioni 1.065 ambazo zimetengwa na WHO kwa ajili ya kutolewa nchini.
Ameongeza kusema kuwa dozi zingine 489,042 zinatarajiwa kuingia nchini siku za hivi karibuni.
Mpaka sasa Tanzania imeshapokea dozi zaidi ya milioni moja ain aya Johnson and Johnson kutoka Marekani.