Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapokea dozi milioni moja ya Sinovac

5b17a5f6a25dad7e99e2be4d7890ee39 Dozi milioni moja chanjo ya Sinovac yatua Dar

Wed, 23 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya imepokea chanjo aina ya Sinovac dozi milioni moja kati ya milioni nne za Ugonjwa wa Virusi vya Corona (Covid-19), ambazo zimetolewa na serikali ya Uturuki kupitia Ubalozi wake hapa nchini.

Akipokea msaada huo leo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kupitia chanjo hiyo, jumla ya watu milioni mbili watachanjwa.

"Hadi sasa tumepokea jumla ya dozi milioni 10.84, ambapo watu wapatao milioni 3.016 tangu tarehe 28 Julai 2021 sawa na asilimia 9.8, huku malengo ikiwa ni kufikia watu milioni 30.74," amesema Ummy.

Ummy ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kupata chanjo ya corona kutokana na kuendelea kuwepo kwa kirusi kipya.

"Nasisitiza watu kuchanja kwa sababu chanjo ndio njia ya uhakika ya kuepuka virusi vya corona," amesema Waziri Ummy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live