Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapokea dawa za minyoo milioni 8

Albendazole (600 X 450) Serikali yapokea dawa za minyoo milioni 8

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

erikali imepokea dawa za kukinga minyoo kwa watoto Albendazole milioni 8 zenye thamani ya Sh550 milioni.

Dawa hizo zilizotolewa na Shirika la Wolrd Vission Tanzania na Canada, zitaanza kugawiwa kwa watoto hao kwenye kampeni maalumu inayotarajiwa kufanyika Juni na Julai mwaka huu.

Msaada huo umepokelewa leo Jumatatu Machi 14 2022 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel wakati wa hafla ya kupokea dawa hizo iliyofanyika katika maghala ya Bohari ya Dawa (MSD).

Naibu Waziri Afya amesema kampeni hiyo ambayo imekuwa ikifanyika mara mbili kwa mwaka Desemba na Juni, husaidia watoto wasiwe na upungufu wa damu, minyoo na kuwa na viini lishe vinavyokwenda kujenga ubongo wa mtoto.

“Tumepokea kitu muhimu sana na dunia ya leo haishindani kwa rasilimali kubwa bali kwa watu wenye akili hivyo hii dawa tunakwenda kutengeneza usalama wa akili za watoto wetu.

“Kimsingi hili tusichukulie tu kama dawa bali tuchukulie zaidi ya dawa na tunapozungumzia masuala ya lishe siyo kushiba sababu wazazi wengi wanachanganya kati ya shibe na lishe ukiwaambie mkalishe watoto wanaenda kuwajaza uji na ugali tumboni.

“Tunamaanisha muwapatie watoto vile viini lishe ambavyo vinakwenda kujenga afya ya mwili na akili ya mtoto ndipo tutakapopata hata wagunduzi na watu wa kushindana kwenye dunia ijayo huu ni usalama wa nchi yetu,” amesema Dk Mollel.

Mjumbe wa Board ya World Vision, Diana Rugaitika alisema kipaumbele cha shirika hilo ni usalama wa mtoto, afya zao na elimu yao alisema walipata nafasi kuchangia dawa hizo mwanzoni mwa mwaka kwa dawa za Sh340 milioni zikiwamo vitamin A na hii ni awamu ya pili.

“Baada ya kuona bado kuna upungufu leo tumepata nafasi tena ya kurudi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa msaada huu ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa na afya njema.

“World Vision Tanzania tukishirikiana na Canada tumeleta Albendazone milioni 8 zinazogharimu Sh550 milioni ambayo tunaamini itaziba kwenye ule upungufu uliokuwepo lakini tunaendelea kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa na afya,” amesema Rugaitika.

Kwa upande wake Balozi Mulamula amesema, “World Vision mmekuwa ni wadau wetu mpo maeneo mtambuka na mmekuwa mkitusaidia katika kuhakikisha watoto wanakuwa salama kiafya, lakini mpo kwenye maeneo mengine na mmetujengea jina nilipokuwa balozi Marekani walikuwa wakisema World Vision Tanzania mko vizuri sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live