Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapambana kuwa na chanjo ya kuaminika

Bbcd96e015b774407e7c4bef2f5b0da8 Serikali yapambana kuwa na chanjo ya kuaminika

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema Tanzania lazima iwe na dawa na chanjo za kuaminika ili kupunguza gharama za kuagiza dawa na chanjo kutoka nje ya nchi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini Kibaha alipotembelea kituo cha chanjo za mifugo ili kujiridhisha kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Serikali imekifadhili kituo hicho shilingi milioni 610 kwa ajili ya kuongeza ubora wa chanjo.

Profesa Ndalichako alisema mifugo ni sehemu ya chanzo cha kipato kwa Watanzania hivyo ni muhimu nchi ikiwa na uwezo wa kutengeneza dawa na chanjo na kuziamini.

“Wizara ina jukumu la kusimamia tafiti hapa nchini ambapo Tume ya Sayansi na Teknolojia imepewa jukumu la kuratibu masuala ya sayansi teknolojia na tafiti ambapo maabara ya kutengeneza chanjo za mifugo ni moja ya vituo vilivyonufaika na fedha za ufadhili toka serikali na ilikipatia kituo hicho kiasi cha shilingi milioni 610,"alisema.

Profesa Ndalichako alisema serikali ilitoa shilingi Sh bilioni 3.2 kwa taasisi zinazofanya utafiti katika kilimo, mifugo afya na viwanda.

"Tumeona baadhi ya vifaa ambapo Wakala wa Chanjo Tanzania wamefanya vizuri na kununua vifaa na kupeleka wataalamu kwenye mafunzo wengine walienda nchi za Nigeria na Ethiopia nimeona fedha zimefanya kazi na wana maabara nyingine haijakamilika,"alisema.

Profesa Ndalichako alisema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiongelea utafiti hivyo wizara itaendelea kufadhili miradi kwa ajili ya tafiti na Costech itaangaalia maeneo ya kipaumbele.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu alisema walitangaza kuratibu miradi minane kwa ajili ya ubunifu ili kuendana na masuala ya uendelezaji wa viwanda na kwamba waliifadhili maabara hiyo ili mifugo ipate chanjo kuongeza ubora.

Chanzo: www.habarileo.co.tz