Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaokoa bil 8.4/- upandikizaji figo nchini

B139ad5e87fde07e6dbda741b9cddad3 Upandikizaji wa figo waokoa mabilioni

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam na Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma kati ya Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu zimetoa huduma ya upandikizaji fi go kwa wagonjwa 14.

Kutokana na matibabu hayo katika hospitali hizo, serikali imefanikiwa kuokoa jumla ya Sh bilioni 8.4 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa hao nje ya nchi, India kupatiwa matibabu hayo ya figo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema hayo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya mwaka 2022/23 ya Wizara ya Afya, bungeni Dodoma jana.

Alisema kwa upande wa Hospitali ya Muhimbili, katika kipindi cha Julai, mwaka jana hadi Machi, mwaka huu imepandikiza figo kwa wagonjwa sita ambapo gharama ya huduma hiyo ni Sh milioni 30 kwa mgonjwa mmoja.

Waziri huyo alisema huduma hiyo hugharimu Sh milioni 120 nchini India. Ummy alisema Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma, kati ya Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu wagonjwa wanane walipata huduma ya upandikizwaji wa figo na kufikisha jumla ya wagonjwa 29 waliopata huduma hiyo tangu hospitali ilipoanza kutoa huduma Machi mwaka 2018.

Alisema gharama ya upandikizaji figo katika hospitali hiyo ni kati ya Sh milioni 27 hadi milioni 35 kwa mgonjwa mmoja ikilinganishwa na Sh milioni 75 hadi milioni 100 mgonjwa mmoja akitibiwa nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live