Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yanunua mitambo ya kuzalisha mitungi 200 ya hewa ya oksijeni

Mitungi Serikali yanunua mitambo ya kuzalisha mitungi 200 ya hewa ya oksijeni

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mitambo hiyo itasimikwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa ya Amana, Dodoma, Geita, Manyara, Mbeya, Mtwara na Ruvuma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameyasema hayo leo Aprili 13, 2021, bungeni wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2021/22.

Amesema hospitali zote saba zimepatiwa mitungi 74 kila moja na kila mtambo mmoja kwenye hospitali hizo utakuwa na uwezo wa kusambaza gesi ya oksijeni katika vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 18.

“Hatua hiyo, inalenga kuimarisha mfumo wa huduma za afya ili kuwa tayari kukabiliana na changamoto za sasa na baadaye,” amesema.

Hata hivyo, amesema maeneo yanayolengwa ni vyumba vya kutoa huduma za dharura, huduma ya mama na mtoto, upasuaji na vyumba vya uangalizi maalum na katika mwaka 2021/22, Serikali itaongeza mitambo mingine ya aina hiyo 12.

Chanzo: ippmedia.com