Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakiri uhaba wa damu

Damu Uptika Ajiii Serikali yakiri uhaba wa damu

Fri, 25 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imekiri kuwepo na uhaba wa damu, huku ikitaja sababu na mikakati iliyowekwa kuondoa hali hiyo.

Akizungumza leo Ijumaa Februari 25, 2022 baada ya kufanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa lengo la kufuatilia hali halisi ya upatikanaji wa damu katika benki hiyo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema makusanyo ya damu yalishuka Desemba na Januari.

Amesema kumekuwa na kushuka kwa kiasi kikubwa Desemba malengo ya benki yalikuwa kukusanya chupa 31,000 lakini zilikusanywa chupa 20,000.

"Kuna taarifa mbalimbali kuhusu upatikanaji wa damu salama nchini, nataka kukiri kwamba ni kweli tuna changamoto ya upatikanaji wa damu salama katika nchi yetu na ni kwa makundi adimu na yasiyo adimu.

“Tumeangalia sababu mbalimbali zilizoleta changamoto lakini kubwa tumeona sababu mbili, upatikanaji wa mifuko ya kukusanyia damu salama na nimewasiliana na taasisi yenye wajibu kuhakikisha mifuko inapatikana ambao ni Bohari ya Dawa (MSD) walinipa sababu ya mlipuko wa Uviko-19 nami nilikubaliana nayo,” amesema Ummy.

Amesema uwepo wa Uviko-19 ulileta changamoto ya upatikanaji wa mifuko hiyo sababu ya usafirishaji huku akitaja changamoto ya pili ni kupungua kwa wachangiaji damu wa hiyari.

Mganga Mkuu wa Dar es Salaam, Dk Radhid Mfaume amesema utafiti uliofanywa Januari mpaka Desemba 2021, takwimu zilionyesha katika kila kina mama 100 wanaofariki kutokana na uzazi 39 sababu kubwa ya vifo vyao ni upungufu wa damu.

“Sababu kubwa ya vifo zimetokana na kutokwa na damu wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua au upungufu wa damu akiwa mjamzito kwa hiyo unaona tukiwekeza kwenye upatikanaji wa damu tutaokoa maisha ya mama" amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live