Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakiri kuzitambua dawa za nguvu za kiume

54603 Pic+bunge

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imekiri kuwepo kwa dawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo haina kemikali, lakini ikasema haijatangazwa rasmi.

Kauli hiyo imetolewa leo, bungeni, Aprili 29,2019 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga (CCM), Godluck Mlinga.

Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alitaja orodha ndefu za dawa za kuongeza nguvu za kiume kisha akahoji kama zina madhara kwa watumiaji.

Awali, mbunge wa viti maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alihoji kama kuna madhara kwa wanaume wanaoongeza maumbile yao pindi wafanyapo mapenzi.

Akijibu, Dk Mwinyi amesema sababu za watu kupungukiwa nguvu za kiume ziko nyingi ikiwemo ugonjwa wa kisukari na msongo wa mawazo, lakini akasema Serikali ilishabaini uwepo wa dawa kwa ajili ya wanaume ambazo hazina kemikali.

Hata hivyo, ameonya matumizi ya dawa ambazo hazijafanyiwa tafiti kuwa si salama kwa matumizi.

Kuhusu dawa za kuongeza maumbile ya uume, Dk Mwinyi  amesema zipo taarifa nyingi za aina hiyo, lakini jambo jema ni kuongeza uelewa wa wananchi ili kutumia dawa zilizothibitishwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz